Alhamisi 5 Novemba 2026 - 06:25
Makamu wa Rais wa Uturuki Ataka Nchi za Kiislamu Ziimarishe Umoja Dhidi ya Israel

Hawza/  Cevdet Yılmaz Makamu wa Rais wa Uturuki, amesema kuwa; ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kusimama kwa msimamo thabiti dhidi ya jinai zinazofanywa na Israel nchini Palestina.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Makamu wa Rais wa Uturuki, Cevdet Yılmaz, katika hotuba yake kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa, amesisitiza kuwa ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kuchukua msimamo thabiti dhidi ya jinai za Israel nchini Palestina.

Cevdet Yılmaz amesema kuwa; kikao cha 42 cha Kamati ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (COMCEC) kinaonesha azma ya pamoja ya kukabiliana na mivutano na migogoro ya kisiasa na kijiografia inayojitokeza katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu, kupitia njia za kidiplomasia.

Yılmaz alitoa kauli hizo alipokuwa akiongoza kikao cha kufunga mkutano wa 42 wa mawaziri wa Kamati ya Kudumu ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Istanbul.

Yılmaz alisema: Licha ya kutangazwa usitishaji vita, kuendelea kwa mauaji ya halaiki, mauaji ya kimbari na jinai za kikatili kabisa zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wenye unaomwaga damu, kwa kutumia visingizio visivyo na msingi kila unapopata fursa, pamoja na kutofikiwa kwa hatua inayofuata ya makubaliano ya usitishaji vita na kuwekwa vikwazo katika njia ya kupeleka misaada ya kibinadamu, kunazidisha kila siku mateso ya ndugu zetu Wapalestina.

Aliongeza kuwa: Sisi kama wanachama wa ulimwengu wa Kiislamu, Waislamu tunapaswa kusimama kwa nguvu zetu zote dhidi ya dhuluma hii na kuiunga mkono Palestina, hususan Ghaza, kupitia hatua na mipango madhubuti.

Chanzo: TRT World.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha